Ijumaa 29 Mei 2026 - 18:00
Iran Bila Kurudi Nyuma, Imeuonesha Ulimwengu Mfano wa Muqawama wa Hussein

Hawza/ Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt nchini Uturuki katika ujumbe wake wa Idi ya Adh-ha, huku ikisisitiza umoja wa Umma wa Kiislamu na kuunga mkono mkondo wa muqawama, imelaani uvamizi wa Israel na Marekani katika eneo hili na kuutaja muqawama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni alama ya kusimama imara dhidi ya ubeberu.

Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt Uturuki kwa mnasaba wa kuwasili kwa Idi tukufu ya Adh-ha imetoa ujumbe ufuatao:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

“Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliye konda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali.”
Surat al-Hajj, Aya ya 27

Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt Uturuki, katika ujumbe wake kwa mnasaba wa Idi ya Adh-ha, imeitaja siku hii kuwa ni Idi ya Waumini ambao kwa roho iliyojaa upendo na huruma, huwasaidia mafakiri, mayatima na wahitaji, na kwa kuwatembelea wakubwa, kuondoa chuki na kuimarisha mafungamano ya kibinadamu, hueneza furaha na mapenzi ndani ya jamii.

Katika ujumbe huu imeelezwa kwamba; Waislamu mwaka huu pia wanaadhimisha Idi ya Adh-ha katika hali ambayo kutokana na kuendelea kwa “mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na Marekani” dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu, mazingira ya Idi yamechanganyika na huzuni pamoja na wasiwasi.

Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt Uturuki, ikirejelea falsafa ya Hijja ya Nabii Ibrahim (as) imesisitiza kwamba; ibada hii ya Mwenyezi Mungu inawaita Waislamu kusimama imara katika safu ya haki, kuwa macho mbele ya nguvu za kibeberu na kuunga mkono mkondo wa muqawama.

Katika sehemu nyingine ya taarifa hii, muqawama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wananchi wa nchi hiyo umetajwa kuwa mfano mashuhuri wa kusimama imara, na imeelezwa kwamba; Iran “bila kurudi nyuma, imeuonesha ulimwengu mfano wa muqawama wa Hussein.”

Jumuiya hii pia imeielezea Hijja kuwa ni alama ya umoja wa Umma wa Kiislamu na kuongeza kuwa; mamilioni ya Waislamu licha ya tofauti za lugha, rangi, mavazi na utaifa, hukusanyika mbee za Mwenyezi Mungu kwa lengo moja, na ikiwa ulimwengu wa Kiislamu utatumia vizuri uwezo huu, Umma wa Kiislamu utarudi tena katika utukufu na mwamko.

Mwishoni, Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt Uturuki huku ikitoa pongezi za Idi ya Adh-ha kwa Waislamu wa Uturuki, mataifa ya Kiislamu na Waislamu wote duniani, iliomba kukubaliwa kwa amali za Mahujaji pamoja na kupatikana kwa umoja na utulivu katika ulimwengu wa Kiislamu.

Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt Uturuki

Istanbul, 26 Mei 2026

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha